Sunday, 28 May 2017

MWAMKO WA VIKUNDI VYA MAZOEZI MWILI (JOGGING CLUB) NCHINI VIGUSE NA HUKU



MWAMKO WA VIKUNDI VYA MAZOEZI MWILI (JOGGING CLUB) NCHINI VIGUSE NA HUKU
Kutana na Kikundi cha mazoezi ya mwili cha Kajima Jogging Club toka Mkoani Mbeya Eneo la Forest mpya kikundi kilichoamuwa kuunga mkono serikali katika suala la wananchi inchini kujitengea muda wa mazoezi ya mwili kwa lengo la kujiepusha na magojwa nyemelezi yasio ambukiza yatokanayo na ulaji wa vyakula na mfumo wa maisha yetu ya kila siku.
Leo hii Mtembezi wetu (mpambanaji) anakutana na Kajima Jopgging Club toka Mkoani Mbeya – Forest Mpya wanaonendelea na ufanyaji wa mazoezi ya mwili kwa kukutana katika mazoezi kwa kila jumamosi.
Jicho la Tatu la Mpambanaji linaona pamoja na mwitikio huo wa vikindi vingi nchini kuanzishwa nchini maeneo mbalimbali imefika wakati sasa vikundi hivyi ni vyema vikajikita pia katika Ujasiriamali na uungaji mkono serikali katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo mfano:- Uanzishwaji wa Club za uhamasishaji utali wa ndani na kutangaza Vivutio vyetu nchini kupitia umoja huu wa Jogging Club. Kwani katika Klabu zetu tuna tunajumuisha watu wa lika tofauti na uwezo tofauti katika kipato na nyasfa hata ajira hivyo ni vyema kusaidiana kwa wale ambao wako mtaani wasio na ajira bado na kuwapa mitazamo chanya ya kiuchumi na kujikwamua kiuchumi.
Wako Mpambanaji niwazo tu.    



Friday, 26 May 2017

UWEKEZAJI KATIKA KILIMO NI CHACHU YA UKUAJI WA TANZANIA YA VIWANDA NCHINI


UWEKEZAJI KATIKA KILIMO NI CHACHU YA UKUAJI WA TANZANIA YA VIWANDA NCHINI

Katika kuelekea katika msingi wa Tanzania ya viwanda, Three Siters Oil Mill Co Ltd kwa Ufadhili wa Shirika la USAID, Technosery, pamoja na Safe wameweza kuwafikia wananchi 600 katika Vijiji vya Kidoka, Mondo, Dalai na Tandala Wilayani Chemba Mkoani Dodoma, kwa kutoa Elimu juu ya Uzalishaji, Uvunaji Bora wa zao la Alizeti na uhifadhi wa malighafi toka shamba kwa kuepuka na kujikinga na SUMUKUVU (Aflatoxins) katika Mazao.
 Habari picha zikionesha wananchi wakipata mafunzo ya uhifadhi bora wa mazao katika vijiji ndani ya Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma.

Bw. Athuman Ally mmoja wa waongozaji toka Three Siters Oil Mill Co Ltd - Dodoma katika moja ya picha katika shamba la Alizeti.

Tuesday, 23 May 2017

DODOMA YENYE KUPENDEZA KWA MAZINGIRA SAFI INAWEZEKANA

Kikundi cha Pambana katika kuunga mkono Serikali yetu ya awamu ya Tano wamezamilia kuung'alisha mji wa Dodoma kwa kupitia Mradi wao wa Ukusanyaji wa Taka za Majumbani. Kupitia Mradi huo kikundi kimeweza kunufaika kiuchumi na kuzidi kujitanua katika uwekezaji ambapo kwa sasa wameweza kumiliki Eneo la Ardhi lenye ukubwa wa Heka mbili ambalo lengo kuu kufanya uwekezaji katika kilimo na ufugaji.

Habari picha hapo chini.

Eneo la Shamba ukubwa wa Heka mbili  ambalo Kikundi kimefanikiwa kumiliki kutokana na kipato toka mradi wa ukusanyaji Taka katika Kaya.



Monday, 15 May 2017

ZAO LA MUHOGO NI FULSA NYINGINE KWA VIJANA NA VIKUNDI VYA UZALISHAJI.

Kicheko kwa wakulima wa Muhongo nchini. Prof, Muhongo kutia saini mkataba wa Tanzania kuuza Mihogo China, Tanzania inatarajia kutia Saini Mkataba wa Kilimo cha Muhogo wa Tanzania kuingia katika soko la China Mei 16 mwaka huu.

Kupitia mkataba huu China italeta wataalamu wa Kilimo cha muhogo nchini kwa ajili ya kutoa ujuzi kwa Wakulima wa Tanzania ili kuongeza uzalishaji. Hivyo basi hii ni Fulsa nyingine kwa wakulima hasa Vijana na Vikundi katika uwekezaji wa Kilimo cha Muhogo nchini.


Watafiti wakiwa katika Shamba lenye mbegu za Mihogo

Sunday, 14 May 2017

IFANYENI BENKI IWAFIKIE WANANCHI WA CHINI PIA

Katika Kuazimisha miaka 50 ya Benki ya Taifa ya Biahara (NBC). Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philipo Mpango aliwaomba wakuu wa Benki hiyo kuona sasa ni namna gani ya Benki hiyo kuisaidia Serikali katika harakati za kuelekea katika Uchumi wa Viwanda nchini kwa Benki hiyo kuweza kuwasaidia Wajasiriamali inchini kwa Uwezeshaji wa Mikopo nafuu wa Riba ndogo. Aidha aliwapongeza watumishi wa NBC kwa ubunifu na kuwekeza katika Mtandao (Kieletronik) katika makusanyo ndani ya Halmashauli nchini.





KUTANA NA FULSA ILIYOWAZI ISIYOTUMIKA

Katika Mipango Mikubwa ya Serikali nchini mmojawapo ni suala la Mazingira, kwani kati ya mambo ambayo serikali ikizembea hujikuta ikibeba mzigo mkubwa kwa kugharamia wananchi wake kwa matibabu na uthibiti wa maambikizi ni mazingira, Uchafuzu na Usimamizimbovu wa mazingira katika maeneo ya kamazi ya watu huleta madhara na majangahini kwa Taifa Serikali kwa kutambua hilo nchini imekuwa ikihamasisha sana wadau na wanaharakati wa Mazingira kujitoa na kuwekeza katika suala la utunzaji wa mazingira. hivyo basi suala la Utunzaji wa Maingira nisehemu nyingine ya Fulsa kwa Vijana katika harakati za Ujasiriamali na uwekezaji.

Kwa kutambua hilo Kikundi cha pambana - Dodoma kimejikita kikamilifu kwa kuunga mkono serikali katika suala la Mazingira kwa kuanzisha mradi wa kukusanyaji taka majumbani kwa kila kaya kuchangia huduma hiyo ya uzoaji Taka. Ni biashara inayolipa na nafuu katika uendesha wake. Nifulsa nyinhine ya kuchangamkiwa.
 Wanakikundi cha pambana wakiwa katika uwajibikaji wa ukusanyajiwa Taka majumbani


 PIcha hapo juu inamwonesha Kati ya wageni waliotembelea Ofisi ya Kikundi mwandishi na mtangazaji Bwana Abdallah Tilata toka Star TV ya Mwanza - Tanzania akisaini katika kitabu cha wageni Ofisini Pambana Group.

 Picha ya juu wageni yoka Kampuni ya simu Airtel Tanzania wakiangalia Bango eneo la ofisi ya Kikundi.


Saturday, 6 May 2017

PAMBANA GROUP : AJALI YAUWA WANAFUNZI KARATU

PAMBANA GROUP : AJALI YAUWA WANAFUNZI KARATU: Gari aina ya Coaster namba haijajulikana lililokuwa limebeba Wanafunzi kuelekea Mjini Karatu kwa Ziara ya kimasomo limepata ajari mbaya na k...

AJALI YAUWA WANAFUNZI KARATU

Gari aina ya Coaster namba haijajulikana lililokuwa limebeba Wanafunzi kuelekea Mjini Karatu kwa Ziara ya kimasomo limepata ajari mbaya na kuuwa wanafunzi waliokuwamo humo kwa idadi kubwa.
 Habari tulizo pata hivi punde toka Hospitali ya Lutherani Karatu Maiti zilizopokelewa hapo Hospitalini ni Maiti 32 yaani Walimu 2, Dereva 1,Wanafunzi wa Kike 18 na Wanafunzi wa Kiume 11.Msafara huo wa wanafunzi ulihusisha mabasi hayo madogo Matatu ambapo moja ndio lilipata ajali hiyo. Suala la uokoaji kwa Wananchi na wasafiri wengine ulihusisha Mashoka, Mitalimbo, Majembe na Vyuma vingine toka kwa wasamalia wema waliojitolea kuokoa maisha wa wahanga hao na Maiti. Tunaendelea kukuletea taarifa hii kila tupatapo habari zaidi

Habari PICHA.














Friday, 5 May 2017

NGUVU YA VIKUNDI KATIKA KUPUNGUZA CHANGAMOTO YA AJIRA INCHINI

Katika kuzingatia na kupunguza tatizo la Ajira inchini, Njia pekee ya kukabiliana na tatizo hili la ajira ni nafasi ya Kujiajiri.
Hata hivyo ukweli nikwamba Changamoto nyingi zinajitokeza zikiwemo Ukosefu wa Mitaji, Mbinu na Ujuzi wa Kujiajiri, ukosefu wa Ubunifu miongoni mwa Vijana wengi inchini. Pia mtazamo kwa Vijana wengi kutaka kujipatia Fedha nyingi kwa Haraka.
Hivyo basi kwakuzingatia hayo nguvu ya Vikundi vilivyo Rasimishwa na kusimamiwa katika misingi madhubuti kunaweza kuongeza ama kutatua tatizo la Ajira inchini kwa nafasi kubwa.
Kupitia haya Nguvu za Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi inawezekana kuwa sehemu ya Suluhisho katika Changamoto ya Ajira kwa Vijana inchini. Elimu itolewe kwa kundi kubwa la Vijana waliopo mtaani wakifikiwa na kuhamasika katika uanzishaji wa:-
1.       Vikundi Rasmi
2.       Uanzishaji wa Kampuni

3.       Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’s)


 UBUNIFU KATIKA KAZI NI TIJA KATIKA KULIKABILI SOKO LA BIDHAA ZAKO


 UDHUBUTU WA KUANZISHA JAMBO AMA MRADI HATA KAMA KIDOGO NDIO MWANZO MZURI WA KUJIJENGA.
 UJUZI.