MWAMKO WA VIKUNDI VYA MAZOEZI MWILI (JOGGING CLUB) NCHINI VIGUSE NA HUKU
Kutana na Kikundi cha mazoezi ya
mwili cha Kajima Jogging Club toka Mkoani Mbeya Eneo la Forest mpya kikundi kilichoamuwa
kuunga mkono serikali katika suala la wananchi inchini kujitengea muda wa
mazoezi ya mwili kwa lengo la kujiepusha na magojwa nyemelezi yasio ambukiza yatokanayo
na ulaji wa vyakula na mfumo wa maisha yetu ya kila siku.
Leo hii Mtembezi wetu (mpambanaji) anakutana
na Kajima Jopgging Club toka Mkoani Mbeya –
Forest Mpya wanaonendelea na ufanyaji wa mazoezi ya mwili kwa kukutana
katika mazoezi kwa kila jumamosi.
Jicho la Tatu
la Mpambanaji linaona pamoja na mwitikio huo wa vikindi vingi nchini kuanzishwa
nchini maeneo mbalimbali imefika wakati sasa vikundi hivyi ni vyema vikajikita
pia katika Ujasiriamali na uungaji mkono serikali katika masuala mbalimbali ya
kimaendeleo mfano:- Uanzishwaji wa
Club za uhamasishaji utali wa ndani na kutangaza Vivutio vyetu nchini kupitia umoja
huu wa Jogging Club. Kwani katika Klabu zetu tuna tunajumuisha watu wa lika
tofauti na uwezo tofauti katika kipato na nyasfa hata ajira hivyo ni vyema
kusaidiana kwa wale ambao wako mtaani wasio na ajira bado na kuwapa mitazamo
chanya ya kiuchumi na kujikwamua kiuchumi.
Wako Mpambanaji niwazo tu.
No comments:
Post a Comment