Habari tulizo pata hivi punde toka Hospitali ya Lutherani Karatu Maiti zilizopokelewa hapo Hospitalini ni Maiti 32 yaani Walimu 2, Dereva 1,Wanafunzi wa Kike 18 na Wanafunzi wa Kiume 11.Msafara huo wa wanafunzi ulihusisha mabasi hayo madogo Matatu ambapo moja ndio lilipata ajali hiyo. Suala la uokoaji kwa Wananchi na wasafiri wengine ulihusisha Mashoka, Mitalimbo, Majembe na Vyuma vingine toka kwa wasamalia wema waliojitolea kuokoa maisha wa wahanga hao na Maiti. Tunaendelea kukuletea taarifa hii kila tupatapo habari zaidi
Habari PICHA.
No comments:
Post a Comment