Kwa mujibu wa Shuhuda wetu ambaye alifika eneo la tukio majira ya saa Tano na dakika 15 usiku na kushuhudia hali ya moto unavyo teketeza mabanda ya wafanyabiashara wadogowadogo wa vifaa vya magari vilivyo tumika, maduka madogo madogo ya bidhaa za Chakula sambamba na mabanda ya Chakula ya Mama Lishe ambapo sehemu kubwa yakiteketea kwa moto mkubwa.
Chanzo cha moto huo inasemekana ulianzia katika mojawapo ya Kibanda cha Mama Lishe kisha kuenea kwa haraka katika mabanda mengine kutokana na upepo uliokuwa ukivuma majira hayo ya usiku, Moto uliendelea kuteketeza mali za Wajasiriamali hao kwa kasi kubwa hasa ukisingatia sehemu kubwa ya bidhaa katika mabanda hayo ilikuwa ni vifaa vyenye mchanganyiko wa mafuta ya mitambo (Oil).
Kamera yetu ilishuhudia juhudi kubwa za Kikosi cha zimamoto cha Mkoa wa Dodoma wakipambana kuzuiya Moto huo kutoenea na kuelekea Eneo la Kituo cha Mafuta kilichapo umbali mfupi toka eneo la mabanda hayo.
Baadhi ya Wajasiriamali waliofika Asubuhi ya leo eneo la tukio kujalibu kuangalia angalau Kitukilicho bakia katika mabanda yao.
Hali ya Moto ilivyokuwa Usiku wa kuamkia leo ulioteketeza sehemu kubwa ya mabanda hayo.
Wamiliki wakipitia pitia asubuhi ya leo kujalibu kuangalia masalia katika mabanda yao.
Moto moto ukiteketeza mali wa Wajasiriamali
Kikosi cha Uokoaji na Zimatoto Mkoa wa Dodoma kikipambana kikamilifu kuzuiya Moto huo usiendelee kuleta madhara katika maeneo mengine
Baadhi ya Wananchi wakishuhudia uharibifu uliotokana na Moto eneo la soko la Miembeni - Majengo Dodoma, Usiku wa kuamkia leo 28/4/2017.
Pambana Group inatoa pole kwa Wajasiriamali wote waliopatwa na mkasa huo tunaamini haitakuwa mwisho wa mapambano ya kutafuta
ReplyDelete